Jeshi la wanamaji wa Australia limekamata boti moja katika pwani ya Oman ambayo haikujulikana inakotoka.
Ilisemekana
ni boti la uvuvi lakini walipofanya upekuzi,wakagundua shehena kubwa ya
silaha ambazo wanashuku zilikuwa zinapelekwa Somalia.Miongozni mwa silaha hizo ni magruneti na bunduki zaidi ya 2,000 za AK 47 bunduki aina za rashasha mbali na bunduki zenye nguvu.
Shehena hiyo ya silaha ilikuwa imefichwa chini ya neti za uvuvi.
Majeshi ya wanamaji wa Australia ni mojawapo ya majeshi ya kimataifa wenye meli zinazoshika doria kwenye bahari kuu na wanamamlaka ya kukamata silaha zinazopelekwa Somalia.
Licha ya marufuku ya Umoja wa mataifa kuzuia kununua ama kuuzwa kwa silaha nchini Somalia ,Umoja huo huwa unairuhusu serikali ya taifa hilo lililosakamwa na vit katika upembe mwa Afrika kununua silaha ndogo ndogo kwa nia ya kuisaidia kujihami dhidi ya makabiliano na kundi la Al Shaabab na kulinda usalama wa raia nchini
No comments:
Post a Comment