Romelu Lukaku ametoboa waziwazi kutoridhishwa na Klabu yake Everton na kuonyesha nia ya kujiunga na Klabu nyingine ili acheze UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Lukaku, ambae Msimu huu amepachika Mabao 25, yupo kambini na Timu ya Taifa ya Belgium ikijitayarisha kucheza na Portugal Jumanne.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amesema hatua nyingine kwenye Soka lake ni kujiunga na Klabu nyingine ili acheze Mashindano ya Ulaya Msimu ujao kitu ambacho Everton, ambao wapo Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England na Pointi 13 nyuma ya Timu ya 4 Man City hawawezi wakikipata Msimu huu.
Huku Baba yake Mzazi akimhimiza ahamie Klabu kubwa kama Bayern Munich na Manchester United, Lukaku amesema hizo ni Klabu ambazo Baba yake anazipenda lakini Wakala wake yupo kazini ambae anashughulikia masuala yake.
Lukaku amehusishwa pia na kurejea Chelsea ambako aliondoka kwa Dau la Pauni Milioni 28 kuhamia Everton Mwaka 2014 lakini mwenyewe ametamka: “Hapana, nitasema hapana kwa hilo. Sina cha kujiridhisha huko. Nilihama na wao wakasonga. Wakatwaa Ubingwa na mimi nikaongeza ubora na sasa tutazame baadae kuna nini!”
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford
1700 Bournemouth v Man City
1700 Norwich v Newcastle
1700 Stoke v Swansea
1700 Sunderland v West Brom
1700 West Ham v Crystal Palace
1930 Liverpool v Tottenham
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton
1800 Man United v Everton
No comments:
Post a Comment