Monday, 21 March 2016

Leo ni Birthday ya Ronaldinho, hivi ni vitu vitano vya kukumbukwa kutoka kwake (+Video)

March 21 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkali wa soka kutokea Brazil Ronaldinho, ambae kwa siku ya leo anasherehekea kutimiza umri wa miaka 36. Ronaldinho kacheza vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya ikiwemo FC Barcelona. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee vitu vitano vya kukumbwa kutoka kwa Ronaldinho.
5- Akiwa na umri wa miaka 13 Ronaldinho aliweka rekodi ya kufunga magoli 23 pekee yake katika mechi moja, rekodi ya Ronaldinho kufunga goli 23 ilimfanya aanze kupata umaarufu akiwa na umri mdogo.
4- Ronaldinho ni miongoni mwa wachezaji wachache duniani waliowahi kushinda mataji yote makubwa ya soka, kama Kombe la Dunia, UEFA, Copa America na mengine mengi.
3- Staa huyo wa Brazil ambae amekuwa maarufu zaidi kutokana skills za kuchezea na kumiliki mpira uwanjani amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara mbili mwaka 2004 na 2005.
BARCELONA, SPAIN - DECEMBER 11:  Ronaldinho holds the Ballon D'or award for European Footballer of the Year on the pitch before the Primera Liga match between Barcelona and Sevilla on December 11, 2005 at the Camp Nou stadium in Barcelona, Spain. (Photo by Denis Doyle/Getty Images) *** Local Caption *** Ronaldinho
Ronaldinho akiwa na tuzo yake ya Ballon d’Or
2- Ronaldinho bado anatajwa kama mmoja wa wachezaji matajiri zaidi kutokea Brazil, hadi December 20 2014 alikuwa anatajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 170.
1- Kama umemiss skills za Ronaldinho unaweza kujikumbusha katika video hii


No comments:

Post a Comment