Sunday, 6 March 2016

HILI NDIYO BAO LA AJIB LILILOIMALIZA MBEYA CITY (Video)

Ibrahim Ajib (aliyepiga magoti) akishangilia bao lake pamoja na Awadh Juma na Danny Lyanga

Ibrahim Ajib (aliyepiga magoti) akishangilia bao lake pamoja na Awadh Juma (kushoto) na Danny Lyanga (kulia)
Wakati mashabiki wengi wa soka wakiwa wanatoka nje ya uwanja wakiamini Simba imeshinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City kwa goli 1-0, striker wa Simba Ibrahim Ajib alipiga bao la pili dkika ya 09+1 na kuumaliza mchezo huo kwa Simba kushinda kwa bao 2-0 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa taifa.
Ajibu alifunga bao hilo baada ya kumtoka beki wa Mbeya City Haruna Shamte na kuachia shuti ambalo lilim-babatiza Hassan Mwasapili na kutinga nyavuni.
Kama ulipitwa na goli hilo bado unayo fursa ya kulitazama kwa mara nyingine kupitia Dauda TV ‘Timu ya Ushindi’

No comments:

Post a Comment