Ipo wazi Diamond anamchango mkubwa kwenye tabia za wasanii waliochini ya label yake ya WCB, ni ngumu kukutana na Diamond Club kama hafanyi show, ndio sababu kubwa huwezi pia kukutana na wasanii waliochini ya label hiyo viwanjani .
“Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda club sitokagi,” amefunguka Harmonize.
Mbali ya kuwa boss wao mwenyewe sio mtu wa viwanja, Harmonize amesema Diamond amewatengenezea mazingira ya kupenda kukaa maeneo ya studio,
“Pale ofisini kuna studio mle mle ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind, kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza kupitia yeye,” alisema Harmonize.
Harmonize pia amedai kuwa hawapendi kujichanganya ili kukwepa skendo zisizo na maana.
Source: EATV
No comments:
Post a Comment