Arsene Wenger amesisitiza Arsenal haijakata tamaa kutwa Ubingwa wa Ligi Kuu England na watapigana hadi mwisho.
Kabla ya Krsimasi, Arsenal waliitwanga Man City na Wachambuzi wa Soka kuwapa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wao wa kwanza wa England tangu 2004 lakini baada ya hapo wameshinda Mechi 3 tu kati ya 12 kati ya Mashindano yote.
Jumamosi Arsenal walitoka Sare 2-2 na Tottenham katika Dabi ya London ya Kaskazini na kujikuta wako Pointi 8 nyuma ya Vinara Leicester City na Pointi 3 nyuma ya Timu ya Pili Tottenham huku wao wakiwa Nafasi ya 3 huku Gemu zikibaki 9.
Wakipaswa kurudiana na Hull City Jumanne Usiku huko KC Stadium kwenye Mechi ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP baada ya kutoka 0-0 huko Emirates, Wenger amekataa kukubali kuwa Kombe hili ambalo wamelitwaa mara 2 zilizopita ndio Taji pekee ambalo huenda wana nafasi nzuri ya kulitwaa.
Mbali ya kuwa Nafasi ya 3 kwenye Ligi ambayo pia huenda wakapokonywa ikiwa Man City watashinda Mechi yao ya kiporo, Arsenal pia wako hatarini kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuchapwa Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano 2-0 na Barcelona ndani ya Emirates na sasa watarudiana huko Nou Camp Wiki ijayo.
Wenger amedai: ”Huwezi kufikiria namna hiyo. Ligi bado haijaisha. Nikukumbushe tu, Leicester tumewafunga mara 2 na hivyo tumefanya kazi yetu. Watu waziangalie Timu nyingine pia. Sisi hatutakata tamaa, tutapigana hadi mwisho!”
Ikiwa Arsenal wataifunga Hull City basi watatinga Robo Fainali ya FA Cup na kucheza na West Bromwich Albion.
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
Raundi ya 5-Marudiano
Jumanne Machi 8
2200 Hull City v Arsenal
Raundi ya 6-Robo Fainali
Ijumaa Machi 11
2255 Reading v Crystal Palace
Jumamosi Machi 12
1800 Arsenal au Hull City v Watford
2030 Everton v Chelsea
Jumapili Machi 12
1900 Man United v West Ham
TAREHE MUHIMU
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016
No comments:
Post a Comment