Mabingwa wa Spain ambao pia ndio Vinara wa La Liga, FC Barcelona, wameshinda 3-1 walipocheza na Sporting Gijon huko Estadio El Molinon kwenye Mechi yao ya kiporo ya Ligi hiyo ya Spain.
Kwenye Mechi hii, Kocha wa Barca, Luis Enrique, alibadilisha Wachezaji 6 toka kile Kikosi kilichoitwanga Celta Vigo 6-1 Majuzi kwa kuwatumia Aleix Vidal na Adriano Correia badala ya Dani Alves na Jordi Alba kama Mafulbeki huku Jeremy Mathieu akianza Sentahafu badala ya Javier Mascherano na Ivan Rakitic akicheza Kiungo badala ya Sergi Roberto, wakati Arda Turan akimbadili Iniesta kwenye Ki
Dondoo:
-Sporting Gijon hawajaifunga Barca tangu 1994 na washakutana mara 15 tangu wakati huo na Barca kushinda mara 13 na Sare 2.
Barca walitangulia kufunga katika Dakika ya 25 kwa Bao la Lionel Messi, hilo likiwa Bao lake la 300 kwenye La Liga na kuweka Historia ya kuwa Mchezaji wa kwanza kupiga Bao hizo.
Sporting walisawazisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Carlos Castro lakini Messi akaandika Bao jingine Dakika 4 baadae.
Luis Suarez akapiga Bao la 3 Dakika ya 67 na kuwapa Barca ushindi wa 3-1.
Barca sasa wamecheza Mechi 24 kama Timu nyingine zote za La Liga na kuongoza wakiwa na Pointi 60 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye Pointi 54 na kisha Real Madrid wenye Pointi 53.
VIKOSI:
SPORTING GIJON (Mfumo 4-2-3-1): Cuellar; Lora, Lichnovsky, Mere, Canella; Mascarell, Cases; Perez, Halilovic, Menendez; Castro
Akiba: Alex Barrera, Guerrero, Alberto Garcia, Isma Lopez, Vranjes, Jony, Ait-Atmane
BARCELONA (Mfumo 4-3-3): Bravo; Vidal, Pique, Mathieu, Adriano; Rakitic, Busquets, Turan; Messi, Neymar, Suarez
Akiba: Ter Stegen, Iniesta, Bartra, Munir, Vermaelen, Dani Alves, Mascherano
REFA: Ricardo De Burgos Bengoetxea
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumatano Februari 17
Sporting Gijon 1 FC Barcelona 3
Ijumaa Februari 19
Levante v Getafe CF
Jumamosi Februari 20
Las Palmas v FC Barcelona
RCD Espanyol v Deportivo La Coruna
Real Betis v Sporting Gijon
Jumapili Februari 21
Celta de Vigo v SD Eibar
Rayo Vallecano v Sevilla FC
Malaga CF v Real Madrid CF
Athletic de Bilbao v Real Sociedad
Granada CF v Valencia C.F
No comments:
Post a Comment