Tuesday, 19 January 2016

Watu 18,000 waliuawa Iraq mwaka 2014


Umoja wa Mataifa unasema kuwa ghasai zinazowakumba raia nchini Iraq ni nyingi huku takriban watu 18,800 wakiuawa kati ya tarehe mosi mwezi Januari mwaka 2014 na 31 mwezi Oktoba mwaka 2015.
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi katika kipindi kama hicho kulingana na ripoti mpya.
Umoja wa mataifa unawalaumu wanamgambo wa islamic state kwa kuendesha ghasia na kuwashikilia watumwa 3,500 wengi wakiwa ni wanawake na watoto.
Kamishina mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za binadamu Zeid Raad Al Hussein anasema ripoti hiyo inaonyesha kile wakimbizi kutoka Iraq wanatoroka wakati wanakimbilia ulaya na maeneo mengine.
Ripoti hiyo inatokana na mahojiano na wale waliohama makwao na ushuhuda wa moja kwa moja kutoka kwa waathiriwa au wale walioshuhudia ukiukaji wa haki za binadamu.
Inasema kwa idadi ya raia 18,802 waliouawa na 36,245 waliojeruhiwa kati ya tarehe 1 Januari mwaka 2014 na Oktoba 31 mwaka 2015 huenda ikawa ya juu.

No comments:

Post a Comment