Wednesday, 20 January 2016

Unatakiwa kufanya vitu hivi hata mara moja kwa mwaka

Image result for MAFANIKIO YA MAISHA

Maisha mafupi sana kuwaza ya jana, kufikiria ulipokosea badala ya kufikiria wapi urekebishe, muda ulionao sasa unaweza kufanya makubwa mengi, mimi naamini katika Ndoto zangu za mafanikio  na najua hazina “Expire date” je wewe unaamini katika nini, tunafanya mengi sana yapo yaliyo na maana na yasiyo na maana nikimanisha faida, ila kuna mambo ambayo unatakiwa ufanye hata mara moja tu kwa mwaka na utajifunza kitu.
Ijadili Furaha yako
Jiulize kama una furaha, na maisha ,kazi, mpenzi wako,ndugu zako au chohote kinachokuhusu na kama hauna furaha ni kwanini na nini kitakachokupa furaha, hii ni kwa faida yako sababu kila mtu anastahili furaha
Jitoe kwa wasio Jiweza
Unakaa ndani na nguo hujavaa miaka miwili unaweka mafurushi ndani, wagawie wengine kuna watu hawana nguo kuna watu hawana viatu wape wanaohitaji, una makabati mawili ya nguo na unava robo ya nguo zote zingine wape masikini.
Tembelea sehemu hujawahi fika
Tembelea sehemu mpya kutana na watu wengine, jifunze lugha au chakula chao hii ni kujifunza kuhusu tamaduni ya watu walio tofauti na asili yako,utajifunza kitu au vitu kutoka kwao .
Fanya uchunguzi wa Kiafya
Tembelea hospitali, na ufanye uchunguzi wa afya yako kwa mwili mzima, afya yako kwa ujumla, achana na mazoea ya kufika hospitali mpaka uwe unaumwa yapo magonjwa yanajificha kama kansa, huwa hayana dalili za haraka.
Tembele kituo Cha Watoto Yatima
Chagua kituo kimoja katika mji wako au mtaa wako, uwe unakitembelea hata mara moja kwa mwaka, kula nao chakula, tengeneza urafiki nao
Jifunze kutumia Uma na Kisu wakati wa kula
Sio utamaduni wa Mtanzania wa kawaida kutumia uma na kisu ila jifunze sababu kujua kitu si sawa na asiye jua kabisa, tembelea migahawa mikubwa na ujifunze kitu tofauti na kwa mama ntilie.
Acha Au punguza kutumia kitu ukipendacho
Kama pombe, soda,kuvuta sigara  au kitu chochote hata kwa wiki uangalie unajisikiaje,
Soma kitabu cha kukujenga kiimani
Soma kitabu cha dini, ambacho ni mara chache unakishika soma kurasa kwa kurasa, jitolee kuwafundisha wengine hasa watoto.
Tumia weekend Moja pekeako
Unatoka na marafiki siku za mwisho wa juma. Basi tumia weekend moja  kuwa pekeako na kufanya yanayo kufuraisha.
Buni Mradi na ufanye ukue
Buni biashara au mkakati itakayo kufanya upime uwezo wako wa kusimama kama wewe, kuwa boss wa maisha yako bila kusimamiwa  na mtu na uendeleze mradi huo.

No comments:

Post a Comment