Umoja wa Mataifa na
mashirika ya kutoa misaada yametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuipa
msaada wa takriban dola 885 milioni kuwasaidia zaidi ya watu milioni
tano wanaohitaji misaada ya chakula nchini Somalia.
Miongoni mwao
wakiwa zaidi ya watoto 310,000 ambao wanakabiliwa na tishio kubwa na
kuangamia kutokana na baa la njaa na utapia mlo ikiwa hawatapata misaada
ya dharura.Mratibu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Somalia Peter De Clrecq, amesema wito huo ni muhimu sana na utasaidi watu wengine milioni moja nukta moja waliokimbia vita nchini Somalia.
Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Baido, Bossaso, Gaalkayo, Kiismayo na mji mkuu wa Mogadishu.
No comments:
Post a Comment