Rafael Nadal
ameondolewa kwenye raundi ya kwanza katika shindano la tenisi la
Australian Open baada ya kushindwa seti tano na Fernando Verdasco.
Hii ni mara ya kwanza kwa Nadal kuondolewa kwenye shindano katika raundi ya kwanza.Wachezaji hao wawili kutoka Uhispania, wanaotumia mikono ya kushoto, walikabiliana katika uwanja wa Rod Laver Arena kwa zaidi ya saa nne na dakika 40.
Verdasco alishinda 7-6 (8-6) 4-6 3-6 7-6 (4-7) 6-2.
Mwanatenisi huyo aliyeorodheshwa nambari 45 duniani sasa atakutana na Dudi Sela kutoka Israel raundi ya pili.
Verdasco alishindwa na Nadal nusufainali za 2009.
No comments:
Post a Comment