Saturday, 2 January 2016
PETER MSIGWA AHITAJI USHIRIKIANO KUTOKA KWA WANANCHI WA JIMBO LA IRINGA
Wakazi wa jimbo la Iringa wameaswa kushirikiana na Mbunge wao katika harakati za kujiletea na kuliletea maendeleo jimbo la Iringa mjini.
Akitoa rai hiyo katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa Mchungaji Peter Msigwa pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa Iringa kwa kuweza kumwamini na kumchagua tena kuwa Mbunge wao.
Mchungaji Msigwa amesema kuwa muda huu sasa si wa kuendelea kujadili kuhusiana na masuala ya uchaguzi kwani muda huo ulishapita na sasa kinachotakiwa ni wananchi wote kuweka kando masuala ya tofauti za kiitikadi na kushirikiana na kujiletea maendeleo.
Amesema kuwa kilichoko mbele yake kwa sasa ni kuhakikisha anatekeleza ahadi alizokuwa ameziahidi katika kampeni za uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment