Saturday, 2 January 2016

MATOKEO YA LIGI YA ENGLAND NA VIDEO ZAKE ZA MAGOLI YALIYOFUNGWA

Image result for PREMIER LEAGUE IMAGE Jumamosi Januari 2
West Ham 2 Liverpool 0           
Arsenal 1 Newcastle 0      
Leicester 0 Bournemouth 0                
Man United 2 Swansea 1          

Norwich 1 Southampton 0                 
Sunderland 2 Aston Villa 1                 
West Brom 2 Stoke 1        

KEPTENI Wayne Rooney Leo ameipa mguu mwema wa kuanza Mwaka Mpya wa 2016 alipoipa Manchester United ushindi kwa kufunga Bao la ushindi walipoifunga Swansea City 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Ushindi huu, ambao ni wa kwanza katika Mechi 8, umeipandisha Man United hadi Nafasi ya 5.
Bao za Man United zilifungwa na Anthony Martial Dakika ya 47 na Swansea
kurudisha Dakika ya 70 kwa Bao la Gylfi Sigurdsson lakini Wayne Rooney, akipokea pasi safi ya Martial, alifunga Bao la ushindi kwa kisigino katika Dakika ya 77.
Bao hilo limemfikisha Rooney Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu England, akiwa nyuma ya Alan Shearer na pia Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora katika Historia ya Man United akiwa na Bao 238, Bao 11 nyuma ya Mshikilia Rekodi, Sir Bobby Charlton.

VIKOSI:

Manchester United: De Gea, Young, Jones, Smalling, Blind, Schneiderlin, Schweinsteiger, Mata, Herrera, Martial, Rooney.
Subs: Romero, Darmian, McNair, Carrick, Pereira, Fellaini, Memphis.
Swansea: Fabianski, Rangel, Fernandez, Williams, Taylor, Britton, Ki Sung-Yueng, Cork, Sigurdsson, Routledge, Ayew.
Subs: Nordfeldt, Naughton, Amat, Grimes, Montero, Barrow, Gomis

REFA: Jonathan Moss

LIGI KUU ENGLAND

Ratiba

Jumapili Januari 3

1630 Crystal Palace v Chelsea                  
1900 Everton v Tottenham     

















No comments:

Post a Comment