"yeyote anaedai kwamba uchumi wa Marekani unadidimia anaota ," rais Obama aliwaambia wabunge mjini Washington.
Hotuba hiyo kwa bunge la Congress ilielezea zaidi mafanikio yake kama vile sera yake ya mageuzi katika sekta ya afya.
Hotuba hii itakumbukwa tu si kwa maelezo yake juu ya sera, lakini pia ni tathmini yake kuhusu namna Marekani ilivyo bora zaidi kuliko Barack Obama alipoingia Mamlakani, anasema mhariri wa BBC wa Amerika kaskazini Jon Sopel
" Katika hotuba ya mwisho kwa bunge hili , sitaki kuongelea a tu kuhusu mwaka ujao . Nataka kuangazia juu ya miaka mitano ijayo , miaka 10 na zaidi,''alisema Obama. " Nataka kuangazia hali yetu ya baadae.''
Alipinga madai ya wanasiasa na wachanganuzi kwamba Uchumi wa Marekani unadhoofika.
Alitoa wito kwa wapiga kura na wanasiasa kubadili kauli zinazotenganisha za kisiasa na ''kubadili mfumo wa kujitathmini wenyewe".
Bwana Obama alisema kuwa suala analojutia zaidi katika utawala wake ni kwamba Republicans na Democrats wamekua maadui baina yao.
"wakati wanasiasa wanapowatusi waislam, wakati msikiti unapoharibiwa kwa maksudi, ama mtoto anapozomewa, hilo halitufanyi kuwa salama,'' alieleza Obama. " Hiyo sio kueleza mambo yalivyo. Ni kosa... Na ni kinyume na vile tulivyo kama taifa''
Pia alitangaza mpango wa utafiti wa matibabu ya saratani utakaoongozwa na makamu wa rais Joe Biden. Pia alizungumzia suala la siaha kwa ufupi
No comments:
Post a Comment