LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumapili Januari 17
Liverpool 0 Man United 1
1915 Stoke v Arsenal
BAO la Kepteni Wayne Rooney, la kwanza kabisa Uwanjani Anfield tangu 2005, Leo limewapa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mahasimu wao Liverpool katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Liverpool walitengeneza nafasi nyingi katika Mechi hii lakini Kipa David De Gea na umaliziaji
Goli hilo lilitokana na Kona ambapo Marouane Fellaini alipiga Kichwa kilichogonga Posti na Mpira kuwahiwa na Wayne Rooney na kutinga.
Hilo ni Bao lake la 5 katika Mechi 4 zilizopita na ni la 176 kwenye Ligi Kuu England ambalo limemfanya sasa awe anashikilia Rekodi ya kuwa Mfungaji wa Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England akichezea Klabu 1 tu akifuatiwa na Thierry Henry mwenye 175 alizofunga akiiichezea Arsenal pekee.
Matokeo haya yameipandisha Man United Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Timu ya 4 Tottenham wakati Liverpool wapo Nafasi ya 9 Pointi 8 nyuma ya TottenhaM
![Wayne Rooney celebrates victory at Anfield with his Manchester United team-mates](http://e2.365dm.com/16/01/16-9/20/wayne-rooney-liverpool-manchester-united-premier-league-victory-celeb-anfield_3401718.jpg?20160117213920)
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Clyne, Toure (Benteke - 81'), Sakho, Moreno; Lucas, Henderson, Can; Milner (Caulker - 90'), Lallana (Ibe - 76'); Firmino
Akiba: Ward, Caulker, Smith, Allen, Teixeira, Ibe, Benteke.
Manchester United: De Gea; Young (Borthwick-Jackson - 42'), Smalling, Blind, Darmian, Schneiderlin, Fellaini; Lingard (Mata - 66'), Herrera (Depay - 72'), Martial; Rooney
Akiba: Romero, Borthwick-Jackson, McNair, Varela, Pereira, Mata, Depay.
![Man Utd's Wayne Rooney (L) celebrates scoring the winner against Liverpool](http://e1.365dm.com/16/01/16-9/20/wayne-rooney-manchester-united-anfield_3401532.jpg?20160117155450)
No comments:
Post a Comment