NOU CAMP Jana ilishuhudia mvua ya Magoli wakati Barcelona inaitandika Mtu 10 Athletic Bilbao Bao 6-0 katika Mechi ya La Liga.
Balaa kwa Bilbao ilianza Dakika ya 4 tu baada ya Kipa wao Gorka Iraizoz Moreno kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumwangusha Luis Suarez na pia kutolewa Penati iliyofungwa na Lionel Messi.
Neymar akafunga Bao la Pili na Barca kwenda Haftaimu wakiwa 2-0 mbele.
Kipindi cha Pili, Luis Suarez alipiga Hetitriki na Ivan Rakitic akaongeza 1 na Barca kushinda 6-0.
Nao Atletico Madrid, wakicheza Ugenini, waliichapa Las Palmas 3-0 na kuzidi kuendelea kuongoza La Liga wakiwa na Pointi 47 kwa Mechi 20 wakifuata Barca wenye Pointi 45 kwa Mechi 19 na kisha Real wenye Pointi 43 kwa Mechi 20.
Matokeo:
Jumamosi Januari 16
Sevilla FC 2 Malaga CF 1
Celta de Vigo 4 Levante 3
Villarreal CF 0 Real Betis 0
Jumapili Januari 17
Real Sociedad 1 Deportivo La Coruna 1
Valencia C.F 2 Rayo Vallecano 2
Real Madrid CF 5 Sporting Gijon 1
Getafe CF 3 RCD Espanyol 1
Las Palmas 0 Atletico de Madrid 3
FC Barcelona 6 Athletic de Bilbao 0
Jumatatu Januari 18
2230 SD Eibar v Granada CF
No comments:
Post a Comment