Rais wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni
ya reli Tanzania (RAHCO) Benhadard Tito.
Mhandisi Tito amelazimishwa kukaa kando ilikufanikisha
uchunguzi katika utaratibu uliotumika wakati wa utoaji wa zabuni ya
ujenzi wa reli ya kati.
Magufuli alichukua hatua hiyo kali baada ya mkutano na wadau wanaohusika na ujenzi wa reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”
Uchunguzi wa kimsingi unaelekezwa kwa utoaji wa zabuni hiyo inayokisiwa kugharimu takriban dola milioni $14. Sasa Magufuli al maarufu "The Bulldozer" ameiagiza
mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua
hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo
endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.Si hao tu walioathirika na amri hiyo ya rais Magufuli, bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) pia imevunjiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment