Tuesday, 22 December 2015

IRAQ MBIONI KUIKOMBOA RAMAD

 Image result for iraq's army



Majeshi ya Iraq yamesema kuwa yanakaribia kuukomboa mji wa Ramadi baada ya kuanzisha mashambulizi makali dhidi ya wapiganaji hao wa IS waliokuwa wakishikilia mji huo tangu mwezi mei mwaka huu.

Maafisa wa vikosi vya serikali ya Iraq wanasema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuzikomboa wilaya kadhaa mahala ambapo mamia ya wanadhaniwa kuwepo.

Balozi wa Iraq nchini Marekani Lukman Faily ameiambia BBC majeshi ya serikali na washirika wake walikuwa katika hatua za mwisho za kushinda vita hivyo vya kuukomboa mji huo.

Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani Colonel Steve Warren amekaririwa akisema kuwa bado kuna kazi kubwa katika mapigano hayo dhidi ya kundi hilo la kigaidi.

No comments:

Post a Comment