Dkt. Owdenburg Mdegella |
WAKATI
waumini wa Dini ya kikristo hapa nchini leo wakiungana na wakristo
wenzao kote ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Yesu
Kristo , Askofu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt.
Owdenburg Mdegella amesifu amani iliyotawala nchini kutoka uchaguzi mkuu
hadi sasa na kuwaomba watanzania kumwombea Rais Dr John Mapuguli kwa
kuleta mabadiliko ya kweli ambayo hata wapinzani walikuwa
wakiyataka.
"Salamu zangu na maelezo yangu ni mafupi kila mmoja anafahamu Burundi na Kenya walifanya uchaguzi na hadi leo hii bado wanauana na maisha yanakuwa magumu......ninyi mnafahamu awamu ya kwanza kuja ya pili tumevuka salama ,awamu ya pili kuingia ya tatu pia salama na awamu ya nne kuingia ya tano ndio tumevuka salama salimini zaidi kuliko awamu nyingine zote.....kwa nilitaka kuasema hata wale waliotumia mabomu na kutumia gharama kubwa wakati wa uchaguzi nafikiri walikuwa wamekosa mazoezi kwa muda mrefu ya kutumia mabomu hayo bila sababu Watanzania ni wapenda amani"
Askofu
Dr Mdegella alitoa kauli hiyo wakati wa ibada hiyo ya christmas
iliyofanyika katika kanisa kuu kuwa hadi hapa sasa Bwana Mungu
ametusaidia na sio amesaidia uchaguzi tuo hata mambo mengine ambayo
tulikuwa tunayataka kwa kuzungusha mikono kuwa mabadiliko sasa
yamekuja.
Alisema kuwa Mungu si kaibadilisha Tanzania na kuipa neema katika uchaguzi mkuu pekee kwani kila mtanzania kwa sasa anaona mabadiliko kawaida ukilinganisha na awali kwani wakati wa kampeni watu walikuwa wakizungusha mikono kama ishara ya kutaka mabadiliko na mabadiliko yameanza kuonekana kwani matajiri walikuwa wamejitajirisha mno na masikini walikuwa wamekumbatia umasikini wao .
"Kulikuwepo pengo kubwa kati ya matajiri na masikini kwani matajiri walijitajirisha zaidi na masikini waliendelea kubaki masikini ila sasa kwa kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli mabadiliko ya kweli yanaonekana "
Askofu Dr Mdegella mbali ya kumpongeza Rais Dr Magufuli kwa utendaji mzuri na baraza lake la mawaziri bado alitaka uzi huu wa kutumbua majibu ambao unaendelea uzidi kukazwa zaidi ili kila mtanzania aweze kufaidi matunda ya nchi yake .
" Sasa ombi langu kwenye watanzania najua Francis Godwin utaandika naomba kila mmoja wetu bila kujali ulimpa kura ama ulimnyima tuzame katika maombi kumwombea Rais wetu ili mabadiliko yaendelee na nchi iwe na amani na maendeleo pamoja na mafanikio ...kwa wale waombolezaji naomba leo kuombeleza kumshukuru Mungu na sisi wote kuungana kumwombea Rais wetu na tarehe 3 Januari 2016 wote kutoa shukurani ya pekee kumshukuru kwa kuvuka salama katika uchaguzi na kuendelea kuona neema hii ya utendaji wa Rais wetu pia kazi ya kutumbua majibu iwe endelevu kwa wakubwa na wadogo ....ukimkamanda mtu mwenye msokoto mmoja wa bangi na kumwacha mwenye gunia la bangi ikome japo sisemi mwenye msokoto mmoja asikamatwe wote washughulikiwi "

Alisema
kuwa watanzania ni watu wanapenda amani na utulivu na ndio maana
wamepata kupita katika wakati mgumu wa uchaguzi mkuu pasipo kutokea
machafuko yoyote.
"
Kati ya vipindi vigumu ambavyo watanzania tumepitia kwa amani na
utulivu ni pamoja na kulinda amani wakati wa uchaguzi mkuu na kuingia
katika sikukuu hii ya chritmas bila amani kuvurugika"
Hata
hivyo alisema kuwa amani hii watanzania tumeipata bure na kuwa kuzaliwa
kwake Yesu Kristo kubisha hodi kwa kila mmoja wetu ili aweze kuingia
ndani ya mioyo ya wote hivyo Kazi kubwa kumfungulia ili aweze kuingia
ndani ya mioyo yetu.
Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela ambae alipata kushiriki ibada hiyo alimpongeza askou huyu Dr Mdegella kwa kumpongeza Rais Dr Magufuli na serikali ya awamu ya tano na kuwa moyo huo wa viongozi wa dini unapaswa kuendelea zaidi kwani kauli zao zinasikilizwa zaidi.
Bw Kasesela alisema amependezwa na askofu huyo kutenga muda wa kuiombea serikali na kudai kuwa kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa serikali ya Dr Magufuli akiwemo waziri mkuu na baraza la mawaziri pamoja na watendaji wengine ni nzuri na kila mtanzania anaiona hivyo zawadi kubwa kwa watanzania ni sala na dua zao
No comments:
Post a Comment