Sunday, 15 November 2015
ZANZIBAR INA WAGONJWA WA KISUKARI 7,000
Daktari bingwa wa kisukari kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja , Zanzibar Faidha Kassim Suleiman,amesema idadi ya watu wanaougua kisukari kisiwani hapa inakaribia 10,000.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani, mtaalamu huyo alisema takwimu zinaonyesha kuwa visiwani hivi vina wagonjwa 7,000 na kwamba idadi hiyo ni kubwa kwa vile inaathiri nguvu kazi ya taifa.
Aliwaambia wadau mbalimbali kuwa mfumo bora wa maisha , unaohusisha kufanya mazoezi, kula kwa wakati na kutumia vyakula vyenye afya ndiyo tiba ya maradhi ya kisukari.
Dokta Suleiman alisema wagonjwa wa kisukari kama watakuwa na mpangilio bora wa kula chakula chenye mboga za kutosha na matunda wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila ya kusumbuliwa na ugonjwa huo.
Alisema waathirika wa kisukari Zanzibar wanaongezeka kwa kasi kubwa kutokana na jamii kutokuwa na mpangilio bora wa chakula badala yake hula vyakula visivyo na faida au tiba mwilini.
Aliwaeleza wananchi kuwa watu wengi wanaougua kisukari hawajaweza kufuata miiko na masharti ya ugonjwa huo ndiyo maana wengi wao hukatwa viungo na wengine kufariki dunia mapema, hata kama wangeweza kuishi kwa kutumia.
“ Zanzibar ina wagonjwa wa kisukari zaidi ya 7,000 kiwango ambacho ni kikubwa kwa vile maradhi haya yanaathiri nguvu kazi ya taifa.”
Maadhimisho hayo ya siku ya kisukari kwa mwaka huu Zanzibar yamekuwa ya aina yake tofauti na siku za awali ambapo, imezoeleka kuwepo kwa sherehe kubwa zenye ngoma na shamrashamra lakini kwa mwaka huu kulikuwa na chakula bora cha asubuhi ambacho wanatakiwa kula wagonjwa wa kisukari , ambacho na wengine walikula.
Kauli mbiu mwaka huu iliuliza ‘ ni mlo gani unaotaki
wa kwa mgonjwa wa kisukari”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment