Mu heshmiwa Job Ndugai |
Kuteuliwa kwa jina la Ndugai ni baada wagombea wengine wawili kujitoa katika kinyang"anyiro hicho cha Uspika ndani ya chama cha CCM .
Waliojitoa katika mchakato huo wa kuchaguliwa katika nafasi ya Uspika ni pamoja na Mhe Abdullah Ali Mwinyi na Dr Tulia Ackson Mwansasu hivyo kupisha nafasi hiyo kwenda kwa Mh Job Ndugai.
Katibu wa itikadi na uenezi taifa Bwana Nape Nauye amesema kukamilika kwa uteuzi huo wa nafasi ya Uspika kunatoa nafasi kwa wabunge wote wa CCM kumfanyia kampeni Mh.Job Ndugai ili aweze kuchaguliwa na wabunge wote katika mkutano wa bunge la kumi na moja linalotarajiwa kuanza hapo kesho mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment