Sunday, 15 November 2015

Na huu ni Wasifu wa Brahimi


Image result for brahimi
Brahimi
Bingwa mtetezi wa tuzo ya Mwanasoka bora wa Mwaka, Yacine Brahimi anapigania kuwa mchezaji wa pili kuhifadi tuzo yake, baada ya Mnigeria Jay Jay Okocha kufanya hivyo kwa kushinda 2003 na 2004.

Kilichomfanya awe katika wachache walioteuliwa mwaka huu kugombea tuzo hiyo ni jinsi alivyoendelea kuwa mafanikio tangu alipojiunga na klabu ya FC Porto alikitokea Granada ya Uhispania Julai 2014.

“Ninazidi kupata uzoefu kwa kucheza dhidi ya timu kubwa,” mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 25 aliambia BBC Sport. “Hii ina maana unajifunza zaidi unafanya kazi kwa bidii kila siku ili uwe bora.”
Ni lazima anajiandaa.

Moja kati ya mafanikio makubwa aliyoyapata ilikuwa mwaka 2014/15 katika harakati za kusaka ubingwa wa klabu Bigwa barani Ulaya alipogaragaza mpira mara 42 na ambapo waliomzidi pekee ni mchezaji wa Barcelona Lionel Messi na Eden Hazard wa Chelsea.

Magoli yake matano yaliisaida Porto kufikia robo fainali ya Klabu Bigwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita.

Na kwa kufufua kumbukumbu ya mwaka 1987 walipofikia fainali ya Kombe la Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Wareno hao waliandika rekodi nyingine kwa kuwabwaga Wajeruman hao waliposhinda mkondo wa kwanza katika robo fainali kwa jumla ya magoli 3 -1. Hata hivyo, walishindwa baada ya kufungwa 6-1 mechi ya marudiano.

Hilo lilikuwa jambo la kukumbukwa katika msimu ambao Porto walimaliza ligi wakiwa nambari mbili, huku Brahimi akifunga magoli saba katika ligi ya Ureno Primeira Liga, na kufikisha jumla ya mabao 13 maisha yake ya uchezaji.

Baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi Porto ilimmulika mwanasoka huyo aliyewahi kuchezea Ufaransa katika michuano vijana ya kimataifa na kuongeza hadhi yake kwa kuongeza kifungu cha kumnunua kutoka euro milioni 50 hadi milioni 60.

Ingawa mchezaji huyu mwenye kasi sana hajafikia mabao aliyoyafunga mwaka jana, ameendelea kung’aa 2015-16 akipokezwa tuzo kadha kama mchezaji bora wa mechi.

Moja kati za hizo ilikuwa ni Septemba katika mechi ya Klabu Bigwa Ulaya wakati Porto ilipoumana na Chelsea na akachangia katika ufungaji wa magoli yote mawili mechi hiyo waliyoshinda nyumbani (Porto walishinda mechi zao 19 za kwanza nyumbani 2015).

Mchezaji huyo aliyetoka akademi inayoheshimika sana Ufaransa ya Clairefontaine tayari ameshapachika magoli saba katika mechi kumi na nne za kwanza alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Akiwa kivutio kwa wengi Brahimi anajitahidi kuifanya Porto iwe na mafanikio kama wachezaji waliomtangulia James Rodriguez, Hulk na Falcao katika moja klabu kubwa katika siku za hivi karibuni.
Kwa uwezo wake wa kugeuka kwa wepesi kumiliki mpira na ufundi wa hali ya juu Brahimi amekuwa akisumbua ngome za wapinzani.

“Sifahamu wachezaji wengi wanaoweza kufanya anachokifanya,” Kocha wa Algeria Christian Gourcuff amesema mwaka huu.

Tishio la mchezaji huyo limedhihirika pale Algeria ilipopoteza mechi dhidi ya Ivory Coast katika robo fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika alipokuwa akikabwa zaidi kila alipokuwa akicheza.

Alichezewa visivyo mara saba wakati Ivory iliposhinda kwa magoli 3-1 na visa hivyo vikiongezeka sana kutoka kwa kiwango cha wastani cha mara 3.7 alizofanyiwa madhambi katika hatua ya makundi, ambako Algeria ilikuwa imeibuka imara kutoka katika kundi la kifo.

Licha ya kushindwa kuchukua kombe Brahimi ameendelea kung’ara kila siku.

No comments:

Post a Comment