Sunday, 15 November 2015

Wasifu wa Sadio Mane


Image result for sadio mane

Sadio Mane

Sadio Mane huenda hakushinda chochote mwaka wa 2015 lakini wakati mshambuliaji huyo wa kilabu ya Southampton alipofunga mabao matatu pekee yake, ndani ya sekunde 176 katika ushindi wa nyumbani wa 6-1 dhidi ya Aston Villa mnamo mwezi Aprili ,alivunja rekodi ya ligi ya Uingereza ambayo huenda ikakaa kwa mda mrefu.

Rekodi aliyovunja ilimilikiwa na aliyekuwa mshambuliaji bingwa wa Uingereza na klabu ya Liverpool Robbie Fowler,aliyoiweka mwaka 1994.

Mabao hayo yaliwavutia wengi ulimwenguni na hivyobasi kumuorodhesha mchezaji huyo wa Senegal ambaye amekuwa mshambuliaji hatari zaidi latika ligi ya Uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliweka rekodi nzuri ya ufungaji mabao tangu alipowasili katika kilabu hiyo ya St Marys kwa kitita cha dola milioni 12 mnamo mwezi Septemba mwaka 2014 kutoka kilabu ya Red Bull Salzburg,ambapo alikuwa ameshinda ubingwa wa ligi na makombe mawili ya ligi hiyo.

Lakini kwa kuwa umaarufu wa ligi ya Austria uko chini mara mbili ya ule wa ligi ya Uingereza,umahiri wake ulitiliwa shaka.

Huku mabao hayo matatu yakivutia vichwa vya habari,ikiwemo uchezaji wake mzuri aliouonyesha dhidi ya Chelsea mnamo mwezi Octoba,ambapo alifunga bao moja na kusababisha jingine katika ushindi wa mabao 3-1, umuhimu wake sasa umebainika.

Mane ambaye anaweza kucheza mahala popote katika safu ya mashambulizi,ikiwemo katika wingi,katikati na mbele iwapo atahitajika,alikuwa mchezaji bora baada ya kuchangia katika kuishinda timu ya Jose Mourinho ambayo ilikuwa inapoteza kwa mara ya saba nyumbani akiwa mkufunzi wake.
Bao lake la kusawazisha dhidi ya Liverpool,ni miongoni mwa mabao matatu ambayo Mane amefunga katika mechi 11 za ligi ya Uingereza lakini pia likiwa miongoni mwa pasi nne.

Amejiimarisha katika kampeni yake ya ligi ya Uingereza,baada kutoa pasi moja baada ya kipindi cha Krisimasi alipofunga mabao 9 kati ya mechi 19.

Mabao 10 aliyofunga yalijumlisha 1/5 ya mabao yote yaliofungwa na Southampton na kuisaidia kilabu hiyo kufuzu katika ligi ya Ulaya kwa mara ya pili tangu mwaka 1980.

Akiwa mwepesi na mwenye kasi ,pamoja na ujuzi wa kutamba na mpira mchezaji huyo alianza kuhusishwa na uhamisho wa kuelekea kilabu ya Manchester United ,licha ya Southampton kukana kupata ombi lolote kutoka kwa mabingwa hao wa zamani wa ligi ya klabu bingwa Ulaya.

Mchezo wake mzuri umemfanya Mane kuorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaowania taji la kila mwaka la BBC barani Afrika kwa mara ya kwanza, akilazimika kusahau yale yaliotokea katika michuano ya Afrika mwaka 2015.

Baada ya kupata jeraha siku 16 kabla ya michuano ya kombe hilo kuanza,ilidhaniwa Mane hatoshiriki katika mashindano hayo ,lakini licha ya kuorodheshwa katika mechi mbili za mwisho hakuweza kuisadia Senegal ambayo iliondolewa katika awamu ya makundi.

No comments:

Post a Comment