VIONGOZI
wa Soka huko Ulaya wamethibitisha kuwa Mechi za Wikiendi za Ligi mbali
mbali pamoja na zile za UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI zitaendelea
kama zilivyopangwa licha ya hali tete ya usalama kufuatia mauaji ya Watu
129 huko Paris Ijumaa iliyopita.
Kufuatia
tukio hilo Mechi kadhaa ziliahirishwa au kufutwa Barani Ulaya na Jana
Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyopangwa kuchezwa huko Hannover kati
ya Wenyeji Germany na Netherlands ilifutwa kutokana na tishio la bomu.
Lakini
Msemaje wa UEFA amethibitisha kuwa Mechi za UEFA CHAMPIONZ LIGI na
EUROPA LIGI za Wiki ijayo zitachezwa kama zilivyopangwa.
Huko
France, imethibitika kuwa Mechi za Wikiendi hii za Ligi zitachezwa kama
Ratiba inavyotaka lakini Mashabiki wa Timu ya Ugenini hawataruhusiwa
kuingia Uwanjani kwa sababu za kiusalama.
Nazo
England na Germany zimethibitisha kuwa Ligi zao, Ligi Kuu England na
Bundesliga, zitachezwa Wikiendi hii kama zilivyopangwa.
Huko
Spain, Rais wa La Liga Javier Tebas, amesema Mechi zote Wikiendi hii
zitachezwa ikiwemo ule mtanange wa El Clasico kati ya Real Madrid na
Barcelona Uwanjani Santiago Bernabeu hapo Jumamosi.
No comments:
Post a Comment