MSILU .COM
ARUSHA TANZANIA.
Wednesday, 18 January 2017
Friday, 30 December 2016
Friday, 21 October 2016
Nguli wa muziki wa afro jazz Kenya Achieng Abura afariki dunia
Mwanamuziki nguli wa nyimbo za mtindo wa Afro Jazz kutoka Kenya Achieng Abura amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta (KNH) jijini Nairobi.Tuesday, 18 October 2016
JUMATANO NOU CAMP: BARCA KUIVAA CITY YA GUARDIOLA!
MOJA ya Mechi za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, za Wiki hii zenye mvuto mkubwa ni ile ya Jumatano huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain kati ya FC Barcelona na Manchester City ikiwa ni Mechi ya Kundi C.
Mvuto mkubwa ni Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, kuiongoza Timu yakekutua Nou Camp mahala ambapo ndio chimbuko lake.
Akiwa na Barca kama Mchezaji, Guardiola alitwaa Ubingwa wa La Liga mara 6 na wa Ulaya mara 1 na alipokuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo alizoa Makombe 14 yakiwemo Mawili ya UCL.
Mara ya mwisho kwa Guardiola kuiongoza Timu nyingine kucheza na Barca huko Nou Camp ilikuwa Msimu wa 2014/15 alipokuwa na Bayern Munich na kuchapwa 3-0 kwenye Nusu Fainali ya UCL.
Kwenye Kundi C la UCL, Barcelona ndio Vinara baada ya kushinda Mechi zao zote 2 za kwanza na Man City wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma baada ya kutoka Sare 3-3 na Celtic kwenye Mechi yao iliyopita.
+++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Barcelona imeifunga Man City Mechi zao zote 4 zilizopita za Mashindano rasmi.
+++++++++++++++++++
Wikiendi hii iliyopita, Man City walitoka Sare 1-1 na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo Wachezaji wao Kevin De Bruyne na Sergio Aguero walikosa Penati zilizookolewa na Kipa na pia hiyo kuwa Mechi yao ya 3 mfululizo kutoka Sare.
Wikiendi, Barcelona waliinyuka 4-0 Deportivo La Coruna huku Rafinha akipiga Bao 2 na Staa wao mkubwa, Lionel Messi, alieanzia Benchi baada ya kuwa nje alipoumia Nyonga, alifunga Bao 1.
Kwenye Mechi na Everton, Guardiola alitumia Mfumo wa 3-4-3 lakini huko Nou Camp ataanza na Mabeki Wanne huku Pablo Zabaleta akianza kama Fulbeki wa Kulia kuchukua nafasi ya Bacary Sagna ambae pia aliikosa Mechi na Everton kutokana na maumivu.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
BARCELONA: Bravo, Mathieu, Mascherano, Pique, Digne, Iniesta, Busquets, Rakitic, Messi, Suarez, Neymar
MAN CITY: Bravo, Zabaleta, Otamendi, Kompany, Clichy, Fernandinho, Gundogan, Sterling, Silva, De Bruyne, Aguero
REFA: Milorad Mažić (Serbia)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Ratiba:
Jumanne Oktoba 18
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Tottenham
CSKA v Monaco
KUNDI F
Real Madrid v Legia Warsaw
Sporting Lisbon v Borussia Dortmund
KUNDI G
Club Brugge v FC Porto
Leicester v FC Copenhagen
KUNDI H
Dinamo Zagreb v Sevilla
Lyon v Juventus
Jumatano Oktoba 19
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku
KUNDI A
Arsenal v Ludo Razgrad
Paris St Germain v Basel
KUNDI B
Dynamo Kiev v Benfica
Napoli v Besiktas
KUNDI C
Barcelona v Man City
Celtic v Borussia Monchengladbach
KUNDI D
Bayern Munich v PSV Eindhoven
FC Rostov v Atletico Madrid
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
Diamond na Harmonize washinda tuzo Marekani
Afrika Mashariki
imekuwa na furaha kubwa wikendi kwenye tuzo za kila mwaka za Jarida la
mziki Afrika, maarufu kama Afrimma Awards baada ya wasanii wa Kenya na
Tanzania kuzoa tuzo tofauti kwenye hafla iliyofanyika Marekani wikendi.
Imekuwa
ni ushindi mkubwa kwa Wasanii wa lebo ya Wasafi kutoka Tanzania,
Diamond Platnumz na Harmonize walioibuka mabingwa kwenye vitengo vyao. Diamond alimshinda Mtanzania mwenzake, Ali Kiba katika kitengo cha mwanamuziki bora wa kiume Afrika Mashariki.
Harmonize, anayezidi kuvuma kwa wimbo wake wa 'Inde' aliomujmuisha Dully Sykes, akitunukiwa tuzo ya Msanii mpya wa mwaka.
Hata hivyo Diamond hakuweza kuhifadhi taji lake la msanii bora wa mwaka aliloshinda mwaka wa 2015 kwani tuzo hiyo ilikwenda kwa Mnigeria Falvour.
Kwa upande mwingine, Kenya ilipata tuzo tatu kupitia Msanii wa nyimbo za injili, Willy Paul, aliyeshinda kitengo cha msanii bora wa injili nalo kundi la Sauti Soul likapewa tuzo ya kundi bora la mwaka.
Mwanamuziki wa kike, Akothee, aliondoka na taji la mwimbaji bora wa kike licha ya mashabiki kutishia kutompigia kura
Sunday, 11 September 2016
Ajibu, Mavugo, waendelea kuchafua rekodi ya Mtibwa mbele ya mnyama
Magoli ya Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo yametosha kuifanya
Simba iendeleze ubabe mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga kwa mara
nyingine tena kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Thursday, 8 September 2016
Hizi ndizo njia za kufanikiwa kibiashara
ILI ufanikiwe katika biashara yako inakubidi uwe na jitihada za ziada.
Kadiri mtu anavyoongeza jitihada katika usimamizi wa biashara yake, ndivyo anavyopata mafanikio.
Inapaswa kutumia jitihada za kiakili na kimwili.
Kadiri mtu anavyoongeza jitihada katika usimamizi wa biashara yake, ndivyo anavyopata mafanikio.
Inapaswa kutumia jitihada za kiakili na kimwili.
Subscribe to:
Posts (Atom)