Sunday, 7 August 2016

Ngao ya Hisani: Mourinho mwenye rekodi mbovu vs Ranieri mgeni wa Wembley



baada ya kusubiri kwa takribani miezi 3, hatimaye ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2016/17 unafunguliwa leo kwa mchezo kombe la Ngao Ya Hisani kati ya washindi wa EPL Leicester vs mabingwa wa FA Manchester United. 


Kuelekea mchezo huu tuangalie takwimu na rekodi mbalimbali zinazohusiana na vilabu hivi. 
 Takwimu na Rekodi 
  • Mechi pekee ya Wembley baina ya United vs Leicester ilikuwa katika fainali ya FA Cup mnamo mwaka 1963, na Manchester United 3-1. 
  • Mechi zote za msimu uliopita za EPL baina ya vilabu hivi viwili ziliisha kwa sare ya 1-1.
  • Jamie Vardy alivunja rekodi ya Premier League ya kufunga katika mechi nyingi mfululizo, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Ruud van Nistelrooy, katika mchezo wao kwanza vs Manchester United mnamo November 2015.

Leicester City

  • Hii ni mara ya kwanza Leicester City wanacheza katika Ngao ya Hisani tangu mwaka 1971, ambapo waliwafunga Liverpool 1-0 katika uwanja wa Filbert Street. Foxers walikuwa mabingwa wa ligi daraja la pili sasa hivi Championship – msimu wa nyuma.  
  • Mara ya mwisho Leicester mwenda Wembley na kushinda ilikuwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi mnamo February 2000, wakiwafunga Tranmere 2-1.
  • Katika mechi 5 zilizopita katika dimba la Wembley – wameshinda mechi 3 na kutoa sare 2.
  • Hii ndio mara ya kwanza Claudio Ranieri ataikochi timu katika dimba la Wembley. 
  • Vardy amefunga mara 1 na kutoa assist ya goli moja akiwa anaichezea England katika uwanja wa Wembley. 

Manchester United


  • Hii itakuwa mara ya 30 kwa Manchester United kucheza mchezo wa Ngao wa Hisani.  Wameshinda kikombe hiki mara 20, mara nyingi kuliko timu yoyote katika Historia ya kikombe hicho.  
  • United wameshinda Ngao ya hisani mara 5 kati 6 walizocheza mara ya mwisho. (2007, 2008, 2010, 2011, 2013).
  • Mechi zao 4 walizocheza Wembley wameshinda zote,  mechi ya mwishi kupoteza ilikuwa fainali ya Champions League vs Barcelona 2011. 
  • Jose Mourinho ameshindwa kushinda Ngao ya hisani mara 3 akiwa kocha wa Chelsea, ukiwemo mchezo wa mwisho wa msimu uliopita vs Arsenal na alifungwa na United kwa penati 2007. 
  • Manchester United wamepoteza mechi moja tu kati ya 15 ya Mashindano yote dhidi ya Leicester, kipigo cha magoli 5-3 mnamo September 2014. 
  • Zlatan Ibrahimovic amecheza mara 1 tu katika dimba la Wembley, akiwa na Sweden πŸ‡ΈπŸ‡ͺ ambao walifungwa 1-0 na England πŸ‡¬πŸ‡§  November 2011

No comments:

Post a Comment