Baada ya mfanya biashara tajiri Afrika Mohammed Dewji kuonesha nia ya kutaka kuweka mkwanja kwenye klabu ya Simba, leo tajiri mwingine wa Bongo na mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amewaomba wanachama wa klabu hiyo wampe timu hiyo kwa muda wa miaka 10 ili aienshe mwenyewe binafsi. Manji ambaye miezi michache iliyopita alichaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, ameomba kupewa klabu na atachukua asilimia 75 za uendeshaji wa klabu huku asilimia 25 zikiendelea kubaki kwa wanachama katika kipindi chote cha miaka 10.
“Nipeni timu na nembo halafu majengo yabakie kwenu ikitokea hasara nitalipa mimi na ikipatikana faida asilimia 25 itakuja kwa klabu, nipeni uhuru na timu yenu mimi najua namna ya kuiendesha ikashindana na Azam FC na gharama za uendeshaji nitalipa pia, jumanne naunda kampuni itakayokuja kupangisha timu ya Yanga kwa miaka 10,” amesema Manji kwenye mkutano wa dharula wa klabu hiyo uliofanyika Diamond Jubilee.
“Katika kipindi cha miaka 10 ikipatikana faida asilimia 25 itakwenda kwa klabu na wanachama na asilimia 75 kwangu, kama itakuwa ni hasara basi itakuwa ni hasara yangu hakuna hasara kwa klabu wala wanachama, tayari nimetuma ombi kwa bodi ya wadhamini waongee na nyinyi na kama tutakubaliana tutaingia mkataba.”
No comments:
Post a Comment