Sunday, 7 August 2016

SUAREZ ASHEREKEA USHINDI WA LIVERPOOL DHIDI YA BARCELONA

Suarez-Liverpool

Luis Suarez ameonekana kufurahishwa na ushindi wa Liverpool wa magoli 4-0 dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley siku ya Jumamosi.

Mshambulizi huyo wa timu ya taifa ya Uruguay alikuwa akicheza dhidi ya klabu yake ya zamani wakati wa mechi za kujiandaa na msimu mpya na kushuhudia timu yake Barcelona ikilala mbele ya timu yake ya zamani.
Magoli ya Sadio Mane, Javier Mascherano (goli la kujifunga), Divock Origi na Marko Grujic yalitosha kuipa ushindi Liverpool.
Suarez alijiunga na Barcelona misimu miwili iliyopita alicheza mechi hiyo kwa dakika 75 na kushangiliwa na mashabiki wa Liverpool waliokuwa wamebeba bango lenye picha na ujumbe wa nyota wao wa zamani.
Baada ya kichapo cha 4-0, Suarez aliingia kwenye mtandao wa Instagram na ku-post picha ya bango lililokuwa limebebwa na mashabiki iliyoambatana na ujumbe kwa mashabiki.
Suarez aliandika: “Ni siku maalum. Asanteni mashabiki wa Liverpool kwa ukariku mliounonesha na mnaounesha kwangu siku zote. You Will Never Walk Alone. Tupambane katika kipindi hiki cha pre-season.”

No comments:

Post a Comment