MABINGWA wa Spain, FC Barcelona, wamewafunga Mabingwa wa England Leicester City 4-2 katika Mechi ya International Champions Cup iliyochezwa huko Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden.
Bao za Barca zilifungwa na Munir El Hadadi, Dakika za 26 na 45, Luis Suarez, 34, na Rafa Mujica, Dakika ya 84.
Bao zote za Leicester zilifungwa na Mchezaji wao mpya kutoka Nigeria Ahmed Musa, alieingizwa Kipindi cha Pili, na kutoboa Dakika za 48 na 66.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Barcelona: Masip; Vidal, Mathieu, Santos, Camara; D. Suarez, Turan, Sergi; Munir, Messi, L. Suarez
Leicester: Zieler; Simpson, Huth, Morgan, Chilwell; Albrighton, Drinkwater, King, Gray; Mahrez, Vardy
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumatano Agosti 3
Barcelona 4 Leicester City 2
Alhamisi Agosti 4
0230 Bayern Munich v Real Madrid
0400 AC Milan v Chelsea
Msimamo
1 PSG Pointi 9
2 Barca 6
3 Bayern 4
4 Chelsea 3
5 Real Madrid
6 Liverpool 3
7 AC Milan 2
8 Leicester 2
9 Celtic 1
10 Inter Milan 0
No comments:
Post a Comment