MECHI SPESHO kwa ajili ya kumtambua na kumuenzi Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney iliyochezwa Old Trafford kati ya Man United na Everton ilimalizika kwa Sare ya 0-0.
Rooney aliingia Uwanjani kuanza Mechi hii akiwa na Wanawe Watatu na kuwekewa Gwaride la Wachezaji wa pande zote na kucheza Mechi kwa Dakika 50 na kisha kupumzika kumpisha Marcus Rashford.
Ilitarajiwa Mechi hi ya Timu mbili ambazo ndizo pekee Rooney amezichezea katika maisha yake ya Soka itakuwa laini lakini mara nyingi Wachezaji wa pande zote mbili walijikita kwa Miguu ngangali.
Kipindi cha Pili cha Mechi hii, Meneja wa Man United, Jose Mourinho, akisimamia Mechi yake ya kwanza Uwanjani Old Trafford, alibadili Wachezaji 6 katika Kikosi chake.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea (Romero 64), Valencia (Darmian 64), Bailly (Jones 46), Blind (Mata 64), Shaw (Rojo 46), Carrick (Schneiderlin 46), Herrera (Fellaini 46), Lingard (Young 46), Rooney (Rashford 53), Martial (Mkhitaryan 46), Ibrahimovic (Memphis 64)
Akiba Hakutumika: Johnstone.
EVERTON: Stekelenburg (Joel 46), Coleman, Baines (Oviedo 65), Funes Mori, Stones, Holgate (Besic 65 (Davies 77)), McCarthy (Gibson 65), Barry (Cleverley 65), Barkley (Lennon 65), Deulofeu (Mirallas 46), Lukaku (Kone 65)
Akiba Hakutumika: Galloway.
HABARI ZA AWALI:
MECHI KUMUENZI ROONEY: LEO OLD TRAFFORD MAN UNITED v EVERTON, KUWEKA HISTORIA YA FACEBOOK!
LEO USIKU Manchester United watajimwaga Uwanjani kwao Old Trafford kucheza na Everton katika Mechi ya Kirafiki maalum ya kumuenzi Nahodha wao Wayne Rooney kwa utumishi uliotukuka wa Miaka 12.
Katika Historia yake ya Soka, Rooney amezichezea Klabu mbili tu na nazo ni Everton alikoanzia na sasa Man United.
Gemu hii itaweka Historia Mpya kwa kuwa ya kwanza kabisa kwa Timu za Ligi Kuu England kuonyeshwa moja kwa moja -laivu- kwenye Mtandao wa Facebook kupitia Kurasa za Wayne Rooney na ule wa Klabu ya Man United na kuweza kuwafikia Watu Bilioni 1.7 Duniani kote.
Mapato yote ya Mechi hii utaenda kwenye Mfuko wa Hisani wa Wayne Rooney ambao lengo lake ni kusaidia Watoto wenye matatizo ya aina mbalimbali.
Mechi hii ni ya kwanza kwa Man United Uwanjani Old Trafford tangu Mwezi Mei walipoifunga Bournemouth na pia ni ya kwanza kwa Meneja mpya wa Man United Jose Mourinho kuongoza Kikosi chake Uwanjani humo.
Rooney, aliesainiwa na Man United Mwaka 2004 akitokea Everton huku akiwa na Miaka 18, ameshaichezea Man United Mechi 520 na sasa amebakisha Bao 4 tu kuikamata Rekodi ya Mfungaji Bora wa Klabu hiyo Rekodi ambayo inashikiliwa na Sir Bobby Charlton aliepachika Mabao 249.
Mara ya mwisho kwa Man United kukutana Msimu uliopita ni huko Wembley kwenye Nusu Fainali ya FA CUP ambayo Man United walishinda 2-1 huku Bao la ushindi likifungwa mwishoni na Anthony Martial.
Kabla, Msimu huo uliopita, Man United iliifunga Everton nje ndani kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni 1-0 ndani ya Old Trafford na 3-0 huko Goodison Park.
Hivi sasa Everton pia ipo chini ya Meneja mpya, Ronald Koeman kutoka Holland, ambae alihamia hapo Mwezi Juni akitokea Southampton.
Kwa Everton, tegemezi lao kubwa ni Straika wao Mrefu, Romelu Lukaku, mwenye Urefu wa Futi 6 Inchi 3, ambae aliwahi kucheza chini ya Mourinho huko Chelsea lakini akatolewa kwa Mkopo kwenda WBA na kisha Everton ambako alinunuliwa moja kwa moja Mwaka 2014.
Msimu uliopita, Lukaku ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Everton akipachika Bao 25.
Kwa Man United, Mechi hii ni fursa nzuri kuwatumia Wachezaji wao wapya Watatu, Eric Bailly, Henrik Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic hasa kwa vile Jumapili watatinga huko Wembley, London kucheza Mechi ya Kufungua Pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa wa England Leicester City.
Je Wajua?
Rooney ashapambana na Everton mara 20 tangu aondoke huko na kujiunga na Man United na kupachika Bao 5.
Ratiba/Matokeo:
Julai 2016
16 Jul Kirafiki: Wigan Athletic 0 Man United 2
22 Jul Ziara 2016: Man United 1Borussia Dortmund 4
25 Jul Ziara 2016: Manchester City==Mechi ilifutwa
30 Jul Ziara 2016: Man United 5 Galatasaray 2
Agosti 2016
03 Aug Wayne Rooney Mechi Maalum: Everton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
07 Aug FA Community Shield: Leicester City [Wembley, Saa 12 Jioni]
Ligi Kuu England
14 Aug: Bournemouth [Ugenini, Saa 9 na Nusu Mchana]
19 Aug: Southampton [Old Trafford, Saa 4 Usiku]
27 Aug: Hull City [Ugenini, Saa 1 na Nusu Usiku]
Septemba 2016
10 Sep: Manchester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]
18 Sep: Watford [Ugenini, Saa 8 Mchana]
24 Sep Premier League Leicester City [Old Trafford, Saa 8 na Nusu Mchana]
KWA WADAU WA MAN UNITED – TAREHE MUHIMU MSIMU MPYA 2016/17
PATA UNDANI: http://www.sokaintanzania.com/spesho-ripota/4045-kwa-wadau-wa-man-united-tarehe-muhimu-msimu-mpya-2016-17
KWA WALE WADAU wakubwa wa Klabu kubwa Duniani Manchester United, kutolewa kwa Ratiba ya Msimu Mpya wa Ligi Kuu England kumewapa matumaini mapya kwa Msimu Mpya chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho.
Wengi wao wamekuwa na matumaini mapya kabisa baada ya kuyapoteza tangu Sir Alex Ferguson astaafu na kumpata David Moyes aliefeli na kisha Louis van Gaal, ambaer licha ya kutwaa FA CUP, alishindwa kuiwezesha Timu kucheza YEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Kabla ya Man United kuanza Msimu mpya wa Ligi Kuu England, watacheza Mechi 2 za Kirafiki huko China dhidi ya Borussia Dortmund na Manchester City na kisha kurejea Old Trafford kucheza na Everton kwenye Mechi maalum ya kumuenzi Kepteni wao Wayne Rooney hapo Agosti 3.
Msimu Mpya wa 2016/17 utaanza rasmi kwa Mechi ya kufungua pazia ya kugombea Ngao ya Jamii Uwanjani Wembley hapo Agosti 7 ambapo Man United, Mabingwa wa FA CUP, watapambana na Mabingwa wa England Leicester City.
Baada ya hapo, Agosti 13, Ligi Kuu itaanza rasmi kwa Man United kuwa Ugenini kucheza na Bournemouth na kisha kurudi Nyumbani Old Trafford kucheza na Southampton.
Septemba 10 ni Dabi ya Manchester ambapo Man City, chini ya Meneja Mpya Pep Guardiola, watatua Old Trafford kucheza na Man United
Pia, Man United, ambao Msimu huo mpya watacheza UEFA EUROPA LIGI, watasubiri kwa hamu Agosti 26 ambapo Droo ya Makundi ya Mashindano hayo itakapofanyika huko Monaco.
MAN UNITED - TAREHE MUHIMU:
22 JULAI: Man United v Borussia Dortmund huko Shanghai Stadium, China
25 JULAI: [Ugenini] Man United v Man City huko Beijing National Stadium, China
3 AGOSTI: Mechi ya Kumuanzi Wayne Rooney v Everton Uwanjani Old Trafford
7 AGOSTI: Ngao ya Jamii v Leicester Wembley Stadium
13 AGOSTI: Mechi ya Ufunguzi Ligi Kuu Ugenini na Bournemouth
20 AGOSTI: Mechi ya Kwanza ya Ligi Old Trafford na Southampton
26 AGOSTI: Droo ya Makundi UEFA EUROPA LIGI
31 AGOSTI: Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho
10 SEPTEMBA: Dabi ya Manchester v Man City Old Trafford.
15 SEPTEMBA: Mechi za Makundi EUROPA LIGI zinaanza
21 SEPTEMBALeague Cup third round.
15 OKTOBA: Mechi Anfield na Liverpool
22 OKTOBA: Mourinho Stamford Bridge kwa mara ya kwanza kuivaa Chelsea.
26 DESEMBA: Mechi ya Boksingi Dei na Sunderland Old Trafford.
2 JANUARI: Mechi ya kwanza Olympic Stadium na West Ham.
7 JANUARI: FA Cup Raundi ya 3 Man United kuanza kutetea Taji
14 JANUARI: United v Liverpool Old Trafford
25 FEBRUARI: Dabi ya Manchester Etihad Stadium
26 FEBRUARI: Fainali ya Kombe la Ligi Wembley
21 MEI: Mechi ya mwisho ya Ligi Ugenini na Crystal Palace.
24 MEI: Fainali ya EUROPA LIGI huko Friends Arena, SJumatanoen, Sweden
27 MEI: Fainali ya FA CUP Wembley
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba kamili:
Jumamosi AGO 13 Bournemouth [Ugenini]
Jumamosi AGO 20 Southampton [Nyumbani]
Jumamosi AGO 27 Hull City [Ugenini]
Jumamosi SEP 10 Manchester City [Nyumbani]
Jumamosi SEP 17 Watford [Ugenini]
Jumamosi SEP 24 Leicester City [Nyumbani]
Jumamosi OKT 1 Stoke City [Nyumbani]
Jumamosi OKT 15 Liverpool [Ugenini]
Jumamosi OKT 22 Chelsea [Ugenini]
Jumamosi OKT 29 Burnley [Nyumbani]
Jumamosi NOV 5 Swansea City [Ugenini]
Jumamosi NOV 19 Arsenal [Nyumbani]
Jumamosi NOV 26 West Ham United [Nyumbani]
Jumamosi DES 3 Everton [Ugenini]
Jumamosi DES 10 Tottenham Hotspur [Nyumbani]
Jumanne DES 13 Crystal Palace [Ugenini]
Jumamosi DES 17 West Bromwich Albion [Ugenini]
Jumatatu DES 26 Sunderland [Nyumbani]
Jumamosi DES 31 Middlesbrough [Nyumbani]
Jumatatu JAN 2 West Ham United [Ugenini]
Jumamosi JAN 14 Liverpool [Nyumbani]
Jumamosi JAN 21 Stoke City [Ugenini]
Jumatano FEB 1 Hull City [Nyumbani]
Jumamosi FEB 4 Leicester City [Ugenini]
Jumamosi FEB 11 Watford [Nyumbani]
Jumamosi FEB 25 Manchester City [Ugenini]
Jumamosi MAR 4 Bournemouth [Nyumbani]
Jumamosi MAR 11 Southampton [Ugenini]
Jumamosi MAR 18 Middlesbrough [Ugenini]
Jumamosi APR 1 West Bromwich Albion [Nyumbani]
Jumanne APR 4 Everton [Nyumbani]
Jumamosi APR 8 Sunderland [Ugenini]
Jumamosi APR 15 Chelsea [Nyumbani]
Jumamosi APR 22 Burnley [Ugenini]
Jumamosi APR 29 Swansea City [Nyumbani]
Jumamosi MEI 6 Arsenal [Ugenini]
Jumamosi MEI 13 Tottenham Hotspur [Ugenini]
Jumapili MEI 21 Crystal Palace [Nyumbani]
**Tarehe zinaweza kubadilika
No comments:
Post a Comment