Monday, 25 July 2016

Shilole adai amefanyiwa udhalilishaji kwenye kivuko cha kigamboni,hiki ndicho alichoandika..


Msanii wa bongo fleva Shilole kupitia akaunti yake ya Instagram amelalamika kuwa amefanyiwa kitu kibaya kwenye kivuko cha kigamboni.

Msanii huyo hakutaja hasa kitu gani amefanyiwa bali alihoji kama nchi inathamini mchango wa wasanii kwenye kuitangaza nchi na kama kuna thamani yoyote ya mtu kuwa kuwa mtanzania ikiwa kuna vitendo kama alichotendewa,hiki ndicho alichoandika.
Uzalendo maana yake nini??
Je kuna thamani yoyote kuwa mtanzania??
Je jitihada zozote zinazofanywa na wasanii kuitambulisha nchi yao zinathaminiwa??
Jana nimetendewa kitendo cha ajabu katika kivuko cha kigamboni na kutendewa udhalili bila kujali kuwa mimi ni mwanajamii nayegusa maisha ya watu.
Muziki ni biashara, lakini pia tuna nafasi yetu katika kuisaidia jamii na kupeleka ujumbe muhimu.
Tusiheshimiwe tunapohitajika na kudharaulika tunapohitaji tuheshimiwe.
Nimeguswa…. Nimeumia.
Someone should act. @paulmakonda @paulmakonda” ameandika Msanii huyo.shishi
Fahamu Tv bado inafuatilia kwa ukaribu nini kimemtokea msanii huyo na tutakujuza zaidi.

No comments:

Post a Comment