Monday, 25 July 2016

PICHA: Pogba na wakala wake, wakati huu ambapo dili lao linatajwa kukamilika


Ni siku moja imepita toka gazeti la AS liandike kuwa dili la Paul Pogba kujiunga na Man United akitokea Juventus litakamilika ndani ya siku mbili, yaani kuanzia July 27 hadi 28, ila July 25 imeripotiwa kutoka thesun.co.uk kuwa dili la Pogba tayari limekamilika bado kutangazwa tu.

Taarifa hizo za dili la Pogba kuwa limekamilika zinapata nguvu baada ya Paul Pogba na wakala wake Mino Raiola kupost picha inayowaonesha wakifurahia maisha, picha ambayo mtandao wa 101greatgoals.com unaitafsiri kama fumbo na inawezekana dili lao likawa limekamilika.
pogba6
Hii ni taarifa kutoka The Sun ambapo inaonesha kama Pogba ni mchezaji wa Man United
Pogba na wakala wake Mino Raiola amepost picha yao ya pamoja wakiwa katika bwana la kuogelea huku wakifurahia, Pogba alihama Man United 2012 na kujiunga na Juventus na sasa wanataka kumrudisha nyota huyo kwa uhamisho wa rekodi, mitandao inaripoti kuwa Man United wamekubali kulipa zaidi ya Pound milioni 100.

No comments:

Post a Comment