Michuano ya Euro mwaka 2016 inazidi kufika mahali ambapo wengi
wanatamani kuona ladha yake. Ubabe na ufundi wa timu vigogo na zile
zenye uwezo wa kawaida.
Sasa hatua ya robo fainali ndio imeisha na kuikaribisha nusu fainali. Wales, Ureno na Ujerumani na Ufaransa tayari wameshatinga nusu fainali na sasa kazi imebaki kwao kutafuta nani wa kuingia fainali.
Moja ya mechi za nusu fainali zinazosubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Ureno na Wales. Najua wengi watajiuliza kwanini isiwe kati ya Ujerumani na Ufaransa kutokana na ukubwa wa mechi?, jibu ni jepesi tu kwamba, huu ni mchezo unaobeba vita ya mafahari wawili wanaokipiga kunako klabu ya Real Madrid, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.
Hii ni hatua ambayo italeta maumivu kwa mmoja kati ya wawili hawa, kwani kwa sasa ni lazima mmoja aondoke ili ampishe mwingine kucheza fainali.
Hawa ni wachezaji ambao ukiwaangalia ndio wenye mchango mkubwa kwenye mafanikio ya hivi karibuni kunako klabu ya Real Madrid, licha ya kwamba Ronaldo ndiye anaonekana kubeba majukumu mengi zaid klabuni hapo.
Wawili hawa wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na rekodi na historia tofauti kabisa.
Akiwa na umri wa miaka 27, Bale anasaidia Wales kushiriki michuano hii kwa mara ya kwanza na kutinga nusu fainali huku Ronaldo akishiriki michuano hii kwa mara ya nne.
Bale mpaka sasa anashika nafasi ya nne katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Wales akiwa na magoli 22, wakati Ronaldo ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Ureno ambapo mpaka sasa ameshafunga magoli 60 akimwacha mbali Pauleta mwenye magoli 47 ambaye ndiye alikuwa akiishikilia rekodi hiyo.
Ronaldo alipata fursa ya kushiriki michuano hii tangu mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 enzi hizo akipata uangalizi wa karibu kutoka kwa wakongwe kama Luis Figo, Nuno Gomez na wengine wengi.
Ni wazi kwamba Ronaldo ameanza kuibeba Ureno mabegani katika miaka ya hivi karibuni baada ya kukabidhiwa kitambaa cha unahodha.
Tuachane na hayo na twende kwenye pointi ya msingi.
Jambo la msingi hapa ni kwamba ugumu, uzito na umuhimu wa mchezo huo unatokana na ufanano wa wawili hawa kwenye klabu yao. Ronaldo akitokea upande wa kushoto huku Bale akitokea upande wa kulia.
Wote wawili kwa kiasi kikubwa kwa sasa wanazibeba timu zao mabegani.
Kwa nyakati tofauti Bale, kwa upande wake amewahi kusisitiza kwamba inahitaji kuwa na njaa ya goli kwa kiasi kikubwa hasa mtu anayecheza safu ya ushambuliaji ili uweze kufikia kilele cha mafanikio katika soka.
Lakini baadhi ya watu wanaliangalia pambano hili zaidi kama vita ya timu mbili, nchi mbili na sio kufocus zaidi kwa wachezaji hao wawili licha ya kuwa na uhusiano mkubwa na mafanikio ya timu zao.
Wachambulizi wa masuala la soka wanawazungumzia hawa watu kwa namna tofauti kuelekea mchezo huu.
Kwa mfano hilo unaweza kuliangalia kwenye mchezo kati ya Wales na Ubelgiji siku ya Ijumaa. Ulikuwa ni mchezo ambao Wales walikuwa na muunganiko na maelewano mazuri. Wanasema kwamba Bales akiwa timu ya taifa anapenda kucheza kitimu zaidi licha ya kwamba ni staa mkubwa kuliko Ronaldo.
Wakati Ronaldo kwa upande wake anacheza zaidi kuibeba timu yeye pake yake, na ndiyo maana anaposhindwa kufanya hivyo mara nyingi timu inashindwa kupata matokeo mazuri.
Wales ya Bale na Ureno ya Ronaldo zinaingia katika mchezo huo zikiwa na rekodi tofauti katika michezo yao iliyopita. Wales wamefanikiwa kufika hatua hii kwa kishindo baada ya kuitwanga Ubelgiji mabao 3-1, huku Ureno wakifika hatua hii kwa kuunga-unga baada ya kuitoa Poland kwa matuta.
Bale anaweza kuwa na faida kubwa zaidi kwenye mchezo huo kutokana na takwimu zake binafsi na timu kumbeba ukilinganisha Ronaldo. Mpaka kufika hatua hii, Ureno hawajapata ushindi wowote ndani ya dakika tisini, hali ambayo ni tofauti kwa wapinzani wao Wales.
Kwa kuangalia takwimu hapo chini utaona nani ambaye ana nafasi kubwa ya kumfunika mwenzie kwenye mchezo wao wa nusu fainali.

No comments:
Post a Comment