Mtoto wa miaka 7 ameaga dunia katika mazingira ya kustaajabisha sana.
Amini usiamini msichana huyo mwenye umri wa miaka 7 amepigwa jiwe na ndovu!Tukio hilo la ajabu lilitokea katika hifadhi ya wanyama mjini Rabat Morocco.
Ndovu huyo alipura jiwe juu ya ua linalozunguka hifadhi hiyo na kwa bahati mbaya likampata mtoto huyo.
Msichana huyo alipelekwa hospitalini lakini akaaga dunia muda mchache baadaye.
Katika taarifa kwa wanahabari wasimamizi wa hifadhi hiyo wametuma rambirambi zao kwa familia ya marehemu na kusema kuwa hilo lilikuwa tukio la kipekee kwani ua huo umetimiza vigezo vyote vya kimataifa ila hio ilikuwa ni ajali tu.
No comments:
Post a Comment