Thursday, 28 July 2016

Uamuzi wa Nay wa Mitego baada ya BASATA kumfungia kwa muda usiojulikana,soma hapa kufahamu zaidi..


Baada ya BASATA kutangaza kumfungia Nay wa Mitego kutojihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana na kumtoza faini ya shilingi milioni moja,msanii huyo amefunguka na kusema kuwa anatarajia kumalizana na BASATA hivi punde kwa kutekeleza masharti waliyompa.

Nay amedai kuwa BASATA wamemwambia arekebishe sehemu za wimbo,kufuata taratibu za BASATA na kulipa faini waliyomtoza vtu ambavyo vipo ndani ya uwezo wake na kuahidi kuwa atatoa video ya kwanza ya wimbo wake huo wa Pale Kati wiki ijayo kwani atakuwa ameshamalizana na BASATA tayari.
Jana tulikuwa na kikao na BASATA tukafikia muafaka kwamba kuna vitu inabidi nivirekebishe pamoja na faini ya shilingi milioni moja..kwa hiyo mpaka kesho nitakuwa nimeshamaliza vitu vyote wanavyovihitaji kwa hiyo biashara itaendelea na tukijaliwa tarehe tatu video ya kwanza ya Pale kati itakuwa inatoka” alisema Nay wa Mitego alipohojiwa na Planet Bongo ya East Africa Radio.

No comments:

Post a Comment