Sunday, 24 July 2016

Jibu la Elizabeth Michael ‘Lulu’ alipoulizwa yeye shabiki wa chama gani cha siasa

Watu maarufu Tanzania wamekuwa wakizungukwa na mambo tofauti kwenye maisha yao haswa linapokuja swala la kutoa ushirikiano flani kwa vyama vya siasa,

Hivi karibuni kwenye mahojiano aliyofanyiwa Lulu ambaye ni mwigizaji mkubwa wa filamu na maigizo Tanzania aliulizwa Yeye shabiki wa chama gani cha siasa?
Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijibu hivi “Mimi sina chama, ndiyo maana hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, sijaonekana kwenye jukwaa lolote. Miye naamini kura ni siri na nilifanya hivyo ili nisifungamane na upande wowote.”
Lulu yupo kwenye ziara ya vyombo vya habari akitangaza filamu yake mpya ya NI NOMA.

No comments:

Post a Comment