Sunday, 24 July 2016

Ruby amjia juu rapper huyu baada ya kuambiwa “anaringa utadhani ni staa”


Ruby amemjia juu Motra the Future baada ya rapper huyo kulalamika kuwa “anaringa utadhani ni staa” baada ya kukataa kutokea kwenye video ya wimbo aliomshirikisha.

Motra alilalamika kuwa muimbaji huyo wa ‘Forever’ alikataa kutokea kwenye video ya wimbo wake wa ‘One day’ aliomshirikisha, Hata hivyo Ruby amedai kuwa yupo busy na shooting ya video zake mbili mpya
“Wao walinambia kuwa wanataka kufanya video,lakini mimi pia ninafanya video zangu mbili ambazo zinanibana,pia jinsi walivyonifata na uongozi wake kana kwamba ilikuwa ni lazima wakati mimi nilifanya kama kumsaidia,sio kwamba alinilipa.” Ruby alifunguka.
motra
Ruby aliongeza kuwa alimsaidia kufanya chorus na hamana ulazima wa kutokea kwenye video
“Who is Motra kusema kwamba ananiforce tuka shoot hiyo video..Mimi nimemsaidia kulikobaki afanye mwenyewe”
Source: FahamuTv

No comments:

Post a Comment