Msanii mkongwe wa Bongo fleva ambaye pia anafahamika kwa vituko vyake mitandaoni, kwenye radio na Tv BABA LEVO ametumia instagram kutoa ya moyoni kuhusu Diamond Platnumz na uwezo wake wakutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi.
“Tutaruka rukaaaaa lakini bado @diamondplatnumz atakuwa ndo mkombozi wa hii sanaa yetu… Kututangaza katufungulia njia katufungulia masoko ya nnje ya tanzania.. Hahahahaa #SIMBA Mi najisemwa ukweli bhana MONDI ni NOUMA japo huko siku za nyuma asha wahi kunikwangua ka korasi kangu hahahaaaa #D_ONE “Baba Levo na Diamond waliwahi kuwa kwenye wimbo wa Kigoma All Staa ‘Leka Dutigite’.
No comments:
Post a Comment