Monday, 13 June 2016

Magufuli awaapisha Nchemba na Tizeba

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba akila kiapo mbele ya rais Magufuli


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.
Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Rais Magufuli ampongeza waziri Nchemba kwa wadhifa wake mpya
Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment