![]() |
Ulevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo |
Waziri wa maswala
ya ndani wa ufaransa , Bernard Cazeneuve, ametoa ushauri kwa wakuu wa
miji mbalimbali wenyeji wa kinyanganyiro cha soka barani ulaya Euro2016,
kupiga marufuku matumizi ya pombe katika maeneo tete siku ya na hata
kabla ya siku ya mechi kufanyika.
![]() |
Wenye mabaa watalazimika kubadilisha mikebe na chupa wanayouzia pombe ilikuzuia madhara yanayotokana na walevi kutumia vyombo hivyo kama makombora |
Shirikisho la kandanda barani ulaya , UEFA, limeonya kuzichukulia hatua ya hata kuwafurusha kutoka mashindano hayo timu za Uingereza na Urusi iwapo mashabiki wao watajihusisha tena na matukio ya ghasia kama ilivyotokea wakati wa mechi yao katika mji wa Marseille .
![]() |
Ulevi unatajwa kuwa ni moja ya vyanzo vya vurugu hizo |
Serikali ya Uingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya Uingereza siku ya Alhamisi.
Bwana Cazeneuve amenukuliwa akisema
![]() |
Uingereza tayari imeahidi kutuma idadi kubwa ya maaskari wa kupambana na fujo kabla ya mechi ijayo inayohusisha timu ya Uingereza siku ya Alhamisi. |
''Tutaweka marufuku ya pombe katika maeneo yote ya umma''
![]() |
Euro 2016: Marafuku ya pombe viwanjani |
alisema bwana Cazeneuve.
No comments:
Post a Comment