![]() |
Omar Mateen |
Shirika la ujasusi
la Marekani- FBI, limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi
katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia moja huko Florida, alikiri
kuunga mkono kundi la kigaidi la IS, lakini hawakumuona kama mtu hatari.
Mateen,
anasemekana kupigia simu mamlaka ya kitaifa ya maswala ya dharura muda
mfupi kabla ya kuanza kuwapiga watu risasi huku akisema kuwa anaunga
mkono kundi la IS.FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.
![]() |
Eneo la mkasa |
Mateen aliendelea kufanya kazi kama mlinzi wa usalama huku akinunua silaha kisheria.
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
No comments:
Post a Comment