Winga mshambuliaji wa klabu ya Man United ya Uingereza Memphis Depay jina
lake limeingia kwenye headlines tena, baada ya kufanya kitendo ambacho
huenda kikawa na maana ya kuashiria yeye kuondoka au kukosa furaha ndani
ya Man United.
Memphis amewashangaza wengi hususani mashabiki wake wa Man United
wanaomfollow katika account yake ya Instagram, baada ya kuona winga
huyo kaamua kufuta picha zote katika Instagram yake zinazohusu Man United ambazo aliwahi kupost na kubakisha moja akiwa na mpenzi wake pekee.
Memphis katika account yake ya Instagram amefollow watu 11 pamoja na account ya Man United pekee, kati ya hao hakuna mchezaji mwenzake wa Man United aliyemfollow, kitu ambacho kimeandikwa na mitandao mingi ya Ulaya kuwa huenda winga huyo anataka kuondoka Man United.
No comments:
Post a Comment