FA,
Chama cha Soka cha England, kimethibitisha Saa ya kuanza Mechi ya
Fainali ya FA CUP ambalo kwa sababu za kiudhamini huitwa EMIRATES FA
CUP.
Pia, FA imetangaza mgao wa Tiketi za Fainali hii kwa Klabu zitakazocheza, Crystal Palace na Manchester United.
Lakini kwa Mashabiki wengi wa Man United watakaotoka Jiji la
Manchester wamekumbwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuwahi Treni ya mwisho
baada ya Mechi hiyo.
Pambano hilo litaanza Saa 11 na Nusu Jioni, Saa za England, na
endapo Mechi hiyo itakuwa Sare baada ya Dakika 90 basi zitapigwa Dakika
za Nyongeza 30 na kisha, ikibidi, Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Hilo litawawia vigumu Mashabiki wa Man United kuwahi Treni za mwisho 3 ambazo zitaondoka Saa 3 Usiku kwa Saa za huko.
Ili kupunguza adha hiyo Klabu ya Man United imepanga kuweka Mabasi
maalum ya bure kuwasafirisha Mashabiki wenye Tiketi za Fainali hiyo.
Kila Klabu imepewa mgao wa Tiketi 28,780 ambazo Bei zake ni kuanzia
Pauni 45, Shilingi 142,900, hadi Pauni 115, Shilingi 365,200.
Kwenye Fainali hiyo imeamuliwa Crystal Palace iwe Timu ya Nyumbani
na hivyo kuvaa Jezi zao za kawaida Nyekundu na Bluu wakati Man United
itahesabika kama Timu ya Ugenini na hivyo kuvaa Bukta Nyeusi na Shati
Nyeupe.
Mbali ya kutwaa Kombe, Mshindi wa Fainali atazawadiwa Fedha Pauni Milioni 1.8 na Mshindi wa Pili Pauni 900,000.
Refa wa pambano hili ameteuliwa kuwa Mark Clattenburg.
No comments:
Post a Comment