Mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya klabu ya FC Bayern Minich dhidi ya Atletico Madrid umechezwa usiku wa Mei 3 2016 katika uwanja wa Alianz Arena Ujerumani, mchezo huo umechezwa Ujerumani huku Atletico Madrid wakiingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa goli 1-0.
Katika mchezo wa marudiano uliochezwa usiku wa Mei 3 2016, FC Bayern Munich
wameondolewa mashindanoni, licha ya kupewa nafasi kubwa ya kutinga
hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hiyo ilikuwa inatokana na
mchezo wa awali kumalizika kwa Atletico kupata ushindi mfinyu katika uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo wa Alianz Arena umemalizika kwa FC Bayern Munich
kuibuka na ushindi wa goli 2-1, ila hiyo haikuisaidia kutinga hatua ya
fainali, kutokana na kutolewa kwa aggregate ya goli 2-2. Magoli ya FC Bayern yalifungwa na Xabi Alonso dakika ya 31 na Robert Lewandowski dakika ya 74, huku goli la Atletico lilifungwa na Antoine Griezmann.
No comments:
Post a Comment