MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Kiungo wao Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 6 hadi 8 lakini hahitaji upasuaji baada ya kuumia Goti walipofungwa 2-0 na Barcelona Februari 23 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Oxlade-Chamberlain, mwenye Miaka 22, alilazimika kuondoka Uwanjani Emirates mara baada ya kufungwa na Barca huku akitumia msaada wa Magongo kutembelea.
Arsenal, ambao walichapwa 3-2 na Man United Jumapili iliyopita huko Old Trafford kwenye Ligi Kuu England, Jumatano Usiku wako kwao Emirates kucheza na Swansea City Mechi ya Ligi.
Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 3 nyuma ya Tottenham na Pointi 5 nyuma ya Vinara Leicester City.
Wakitoka kwa Swansea City, Arsenal wana kibarua kigumu huko White Hart Lane kwenye Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao wa Jadi, Tottenham hapo Jumamosi Machi 5.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
Jumanne Machi 1
[Mechi zote kuanza 2245]
Aston Villa v Everton
Bournemouth v Southampton
Leicester v West Brom
Norwich v Chelsea
Sunderland v Crystal Palace
Jumatano Machi 2
2245 Arsenal v Swansea
2245 Stoke v Newcastle
2245 West Ham v Tottenham
2300 Liverpool v Man City
2300 Man United v Watford
Jumamosi Machi 5
1545 Tottenham v Arsenal
[Mechi zote kuanza Saa 1800]
Southampton v Sunderland
Man City v Aston Villa
Chelsea v Stoke City
Everton v West Ham
Swansea City v Norwich City
Newcastle v Bournemouth
Watford v Leicester City
Jumapili Machi 6
1630 Crystal Palace v Liverpool
1900 West Brom v Man United
No comments:
Post a Comment