Mchezo huo namba 3, unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa saa 10
kamili jioni katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, huku
kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu tatu kwa jukwaa kuuu.
Waamuzi wa mchezo huo ni Lidya Tafesse, akisaidiwa na
Yehuzewdubizua Yehuw, Tsige Sisay, Woinshetkassaye Abera kutoka nchini
Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo huo Geneviev Kanjika akitoka Congo DR
wote wanatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi mchana kwa shirika la ndege
la Kenya (KQ).
Wakati huo huo kikosi cha Twiga Stars kimeendelea na mazoezi
kujiandaa na mchezo huo wa siku ya Ijumaa, huku kocha mkuu wa timu hiyo
Nasra Juma akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na tayari
kuwakabili Wazimbambwe.
Aidha Kocha Nasra amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini na
watanzania wote kwa ujumla, kujitokeza uwanjani siku ya Ijumaa kuja
kuwapa sapoti katika mchezo huo, ambapo watakua wakiwakilisha na
kupeperusha bendera ya Tanzania.
IMETOLEWA NA TFF
No comments:
Post a Comment