Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger amesema wachezaji wa Arsenal sharti wamnyamazishe Luis
Suarez ndipo waweze kuwashinda Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya.
Arsenal watakuwa wenyeji wa Barca mechi ya mkondo wa kwanza katika hatua ya 16 bora Jumanne.Barcelona, chini ya Luis Enrique, wamecheza mechi 32 ligini na katika kombe bila kushindwa, na Suarez amewafungia mabao 12 katika mechi saba alizocheza majuzi.
"Suarez ni mchezaji anayeweza kuunda moyo fulani kwenye timu,” amesema Wenger, aliyejaribu kumnunua Suarez Julai 2013 mchezaji huyo alipokuwa Liverpool.
Washambuliaji wenzake Suarez, Lionel Messi, 28, na Neymar, pia huenda wakashirikiana safu ya mashambulizi dhidi ya Arsenal uwanjani Emirates.
Suarez, 29, ndiye anayeongoza kwa ufungaji mabao La Liga akiwa na mabao 25 na Wenger ameongeza: “Ni lazima tumnyamazishe Jumanne jioni.
“Ninaamini kando na ustadi wa kibinafsi wa washambuliaji hao watatu, huwa wanaelewana sana na kucheza vyema pamoja.
"Ninaamini Suarez husaidia sana timu. Alifanya hivyo akiwa Liverpool, na vile vile akicheza na Edinson Cavani na Diego Forlan [timu ya taifa ya Uruguay].
No comments:
Post a Comment