Taarifa kutoka
vyombo vya habari vya somalia zinasema kuwa Waziri mkuu wa nchi
hiyo,Abdirashid Sharmarke,amekamatwa juzi katika kiwanja cha ndege cha
Nairobi nchini kenya wakati akiwa anafanyiwa ukaguzi wa usalama.
Taarifa
hizo zinasema kuwa afisa usalama aliamuriwa kuacha ukaguzi huo kwa
sababu ndege hiyo ya kukodisha ya Somalia ilikuwa haijafanyiwa ukaguzi
wa lazima katika uwanja wa ndege wa kikanda katika kiwanja cha ndege cha
Kenya.hata hivyo ripoti hiyo inasema ndege iliamua kuondoka na kuwaacha maafisa hao wakiwa wameshikiliwa kwa saa kadhaa.
Kenya imekuwa ikiisalidia somalia kupambana na kundi la kigaidi la la al-shabab lakini katika nchi zote mbili kumekuwa na mvutano baina ya serikali mbili juu ya kundi hilo al shabab na kusababisha mauaji ya baadhi ya askari wa kenya kuuawawa Somalia mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment