Baada ya Mechi 25 kwa kila Timu, huku Mechi zikibaki 13, Barca wapo kileleni wakiwa na Pointi 63 wakifuata Atletico wenye Pointi 55 na ya 3 ni Real yenye Pointi 54.
Mechi zinazofuata kwa Vinara hao ni Jumamosi Februari 27 kwa Dabi ya Madrid kati ya Real na Atletico ndani ya Santiago Bernabeu na Jumapili Barca kuwa kwao Nou Camp kucheza na Sevilla.
Katika Mechi nyingine ya La Liga hapo Jana, Kikosi cha Mchezaji wa zamani wa Man United, Gary Neville, cha Valencia, kiliambua ushindi wao wa pili mfululizo kwenye Ligi hiyo baada ya kuipiga ugenini Granada 2-1 na huu ni ushindi wa 3 mfululizo kwao baada ya pia kuitwanga Rapid Vienna 6-0 Alhamisi kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Wikiendi iliyopita Valencia ilishinda Mechi yao ya kwanza ya La Liga tangu Novemba na Jana walitangulia 2-0 kwa Bao za Parejo, Dakika ya 55, na Mina Lorenzo, Dakika ya 90 lakini Dakika ya 93 Granada walifunga Bao lao 1 kupitia Mendez Ortega.
Ushindi huu umewaweka Valenzia Nafasi ya 11 katika La Liga.
La Liga
Ratiba/Matokeo:
Jumapili Februari 21
Celta de Vigo 3 SD Eibar 2
Rayo Vallecano 2 Sevilla 2
Malaga CF 1 Real Madrid 1
Athletic de Bilbao 0 Real Sociedad 1
Granada CF 1 Valencia 2
Atletico de Madrid 0 Villarreal CF 0
Ijumaa Februari 26
2230 Eibar v Las Palmas
Jumamosi Februari 27
1800 Real Madrid v Atlético Madrid
2015 Sporting Gijón v Espanyol
2015 Getafe v Celta de Vigo
2230 Real Betis v Rayo Vallecano
Jumapili Februari 28
0005 Real Sociedad v Málaga
1400 Villarreal v Levante
1800 Valencia v Athletic Club
2015 Deportivo La Coruna v Granada
2230 Barcelona v Sevilla
Jumanne Machi 1
2300 Atlético Madrid v Real Sociedad
Jumatano Machi 2
0001 Las Palmas v Getafe
2200 Málaga v Valencia
2200 Athletic Club v Deportivo La Coruna
2200 Celta de Vigo v Villarreal
2200 Sevilla v Eibar
2300 Levante v Real Madrid
Alhamisi Machi 3
2200 Granada v Sporting Gijón
2230 Espanyol v Real Betis
2300 Rayo Vallecano v Barcelona
Amazing fact regarding La Linga, CHristiano is my fav, A debt of gratitude is in oder of sharing this post .
ReplyDelete