Mawaziri
wa Magufuli wameendelea kumiliki vichwa vya habari kutawala katika
Wizara mbalimbali Tanzania ambapo leo imegusa katika Wizara ya Nchi,
Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambapo Waziri wake Angellah
Kairuki ametangaza kuwaondoa kazini watumishi watatu kwa ubadhirifu wa
mali za Umma.
Amesema ‘namsimamisha kazi Said Nassoro
aliyekua mkuu wa chuo cha utumishi wa Umma kwa kushindwa kusimamia
watumishi walioko chini yake na kushindwa huko kusimamia kikamilifu,
kumepelekea shughuli za matawi ya chuo hiki mikoani kuathirika na kutoa
mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhirifu wa mali za
umma’
‘Kuanzia mwaka 2011 mpaka 2013 mkuu wa chuo tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la gorofa mbili katika tawi letu la chuo huko Mtwara, CAG na TAKUKURU
walithibitisha ubadhirifu huu lakini mkuu huyu wa chuo niliyemsimamisha
hakuchukua hatua na badala yake alimuhamishia Ngata Tabora na kuendelea
na wadhifa wake’
Waziri Kairuki ameeleza pia ‘Ngata naye anazimamishwa kazi, na wa tatu ni Mbwilo Joseph ambaye mwaka 2013 alitumia vibaya pesa za malipo ya ada Bilioni moja zilizolipwa na Wanafunzi ambapo pamoja na ubadhirifu huo kugundulika bado mkuu wa chuo Nassoro alimteua kuwa kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa utawala na fedha, naye kuanzia leo anasimamishwa’
Mtazame Waziri Angellah Kairuki kwenye hii video hapa chini
No comments:
Post a Comment